Hello world!

“Je tunaijali hadhi yetu na yawenzetu?”

Juzi tu hapa nchini Kenya, tuliona video ambazo zinatuhuzinisha mpaka sasa hivi,makosa ni ya nani?
Mabanati ama marijali?
Vazi langu chaguo langu!! Naam sikatai,lakini dada zangu tunapovaa vijiminisketi vidogodogo tukawaonyesha hawa wanaume mapaja yatu yakawavutia na hatimaye kututamani, makosa ni ya nani? Wakatumia nguvu kututhulumu kwa nia yoyote ile, nani tutakaye muadhibu?
Wala asinipate vibaya mtu, siwatetei hao madhalimu ! LA!Ninachosema nikuwa sisi mabanati ni lazima tujiheshimu na tuvae mavazi yatakayo tupa stara. Nani aliyesema kuwa urembo nikujionyesha. Wataka kusema wavaao nguo zenye heshima si warembo ama hawapati wapenzi wa roho. LA!! Tuhakikishe kuwa vazi tunalo livaa wote wamerithia.
Na sisemi eti watu wasing’are . La!!
Na hao waonevu, makatili, madhilimu haifai kabisa kuonea wanyonge. Kama mwanadada amevaa vazi lisilo la adabu kuna njia mwafaka zilizokubalika za kumrekebisha. Si ati kuwa una nguvu kumshinda wafanya utakavyo. Kumbuka kuwa kila aliye na nguvu hakosi alo Zaidi yake. Na swali ni je? Unapo mvua nguo mwenzio eti sababu yu nusu uchi, umemsitiri au wazidi mwanika faraghani?
Sayari hii ya dunia haiishi kuwa na vituko na balaa kila uchao. Sijui twaiga mila ya kina nani. Waafrika sisi yaonekana kuwa hatujaridhia maumbile yetu. Si rangi tushajipausha, tukajitia nywele za farasi, tukavaa nguo zinazotukosesha maana mbele za wenzetu. Haifai dadazangu…!
Mwafrika ni mtu aliyeumbwa akaumbika, rangi bora Zaidi, asili bora Zaidi, msokoto wa nywele maridadi, aliyesema nani? Si mimi! Mwamjua,mshamsikia pia. Tyra banks. Kwa hilo ng’ara, jitengeneze, jipambe lakini usibadili maumbile yako… hakuna aliye kama wewe, anayevutia na kupendeza. Jipende ili upendwe. Na uwe marithia alivyokuumba muumba.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s